Ngoma ya ‘Not like Us’ ya Lamar inastahili kuwania Grammy

Ngoma ya ‘Not like Us’ ya Lamar inastahili kuwania Grammy

Mkurugenzi Mtendaji wa tuzo maarufu Marekani za Grammy,  Harvey Mason Jr ameweka wazi kuwa wimbo wa ‘Rapa’ Kendrick Lamar wa ‘Not Like Us’ unastahili kuteuliwa kuwania tuzo hizo zinazowapa heshima wasanii nchini humo.

Kwa mujibu wa Tmz ilizungumza na mtendaji huyo ambapo alidai kuwa haoni sababu yoyote kwa nini wimbo huo usiteuliwe au kuchukua tuzo ya Grammy.

“Sioni sababu yoyote kwa nini ‘Not Like Us usiteuliwe au kuchukua Grammy ni wazi ni rekodi ya moto ni msanii wa kushangaza sana huu wimbo ni wa ajabu sana” amesema Mason Jr

Aidha aliongezea kwa kuweka wazi kuwa ‘rapa’ huyo anahistoria nzuri na wapiga kura katika tuzo hizo kwani amewahi kushinda tuzo 17 kati ya teuzi 50 kwa miaka kumi iliyopita huku akitaja kuwa hayo ni mafanikio makubwa sana kwake.

Lamar aliuachia wimbo wa ‘Not Like Us’ kwa ajili ya kumchana ‘rapa’ Drake ukiwa ni muendelezo wa bifu lao la kutoleana povu kupitia ngoma walizokuwa wakiziachia huku wimbo huo ukishika nafasi ya kwanza katika chati za Billboard Hot 100 siku chache tangu kuachiwa kwake.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags