Ngoma kumi bora za Zitto Kabwe 2024

Ngoma kumi bora za Zitto Kabwe 2024

Kama ilivyo kawaida kwa baadhi ya watu mashuhuri, kila ifikapo mwisho wa mwaka huachia orodha ya ngoma walizopenda kusikiliza kwa mwaka mzima.

Aliyekuwa kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameachia mkeka wake ukiongozwa na wimbo wa Diamond aliomshirikisha Zuchu 'Raha'.

Katika orodha hiyo iliyoachiwa na Zitto kupitia ukurasa wa X (zamani Twitter) namba moja na mbili ni kutoka WCB. Baada ya 'Raha' wimbo wake pendwa namba mbili ni 'Pwita' Zuchu, 'Kipofu' Chege ft Alikiba, 'Yule' Ay ft Marioo, 'Mapozi' Simba ft Blue & Jay Melody, 'Natamba Naye' Phina, 'Dah' Nandy ft Alikiba,'Huku' Alikiba & Tommy Flavor, 'Zamani' Founder na namba kumi imeshikwa na Chino Kidd wimbo 'Yesa'.

Kupitia orodha hiyo yupo msanii chipukizi Founder anayekuja vizuri kwenye gemu, hii inaonesha kuwa mwaka 2025 kijana huyo akitupiwa jicho anaweza kufanya makubwa kwenye tasnia.

Founder hadi sasa ameachiwa ngoma kama vile Dar es salaam, Nitatokaje, Niepushe na nyinginezo. Utakumbuka msanii huyo alianza kutambulika baada ya kipande cha video yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii akiimba wimbo wake ‘Nitatokaje’.

Kupitia video hiyo alikuwa akiimba mashairi yanayoeleza kuwa anataka kuwa na brand kama Diamond ndipo meneja wa msanii huyo Babu Tale aliamua kumsaidia katika muziki na kumsomesha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags