Nedy Music: Nimejipanga kiushindani 2024

Nedy Music: Nimejipanga kiushindani 2024

Msanii wa Bongo Fleva, Nedy Music amesema wimbo wake aliomshirikisha Barnaba unaoitwa Mapenzi, umemfungulia njia kwa mwaka 2024.

Amesema wimbo huo una ujumbe mzito na tangu autoe una siku sita na anauona unafanya vizuri kwenye mitandao ya kijamii.

"Mwaka 2024 nimejipanga kiushindani kuhakikisha nyimbo zangu zinaishi kwa jamii, pia mitandao ya kijamii inatupa picha kujua mashabiki wetu wanapenda kitu gani,"amesema na kuongeza

"Inahitajika akili kubwa kupromoti nyimbo, kutokana na kiki zilizopo, kwani wengine hayo siyo mambo yetu, mashabiki walitupenda kutokana na muziki."

Wimbo wake wa Nigee anautaja ndiyo ulikuwa bora kwa upande wake mwaka jana"Kwanza niliisikiliza sana kabla ya kuitoa, baada ya kuitoa naisikiliza hadi leo, ujumbe wake unanigusa."
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags