Ne-Yo kumuoa tena Crystal baada ya kutengana

Ne-Yo kumuoa tena Crystal baada ya kutengana

Aisee mara nyingi suala la kuachwa kwa mke na baadaye kurejewa tena hii bahati hua inawakuta watu wachache tu na hili limedhihirika kwa Muimbaji kutoka nchini Marekani Neyo ambaye amefunga ndoa kwa mara ya pili na Crystal Smith.

Crystal amethibitisha hilo kwa ku-share clip fupi ya harusi yao iliyofanyika siku ya Jumapili usiku Sin City, Vegas.

Hata hivyo kwa mara ya kwanza wawili hawa walidumu kwenye ndoa yao kwa muda wa miaka minne (4) ambapo walikuja kuachana 2020, na baadae kurudiana mwaka 2021 na kisha mwaka huu kufunga ndoa tena kwa mara ya ya pili.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags