Ne-yo akamilisha taratibu za talaka

Ne-yo akamilisha taratibu za talaka

Mwimbaji nchini  marekani  Shaffer Chimere Smith  maarufu kama NE-YO  tayari amekamilisha taratibu zote za talaka na kumlipa aliekuwa mkewe, Kwa mujibu wa makubaliano ya Talaka.

Nyota huyo  atabaki na Nyumba 3 kati ya 4 walizokuwa nazo, na kiasi hicho cha Fedha atalipwa mzazi mwenzake Crystal Renay,  ili kuweka usawa katika Mali isiyohamishika

Renay atalipwa Tsh. Milioni 46.7 kwaajili ya gharama za kuhama, Tsh. Milioni 350.5 za kununua Gari jipya na atabaki na Gari aina ya Bentley Bentayga ya Mwaka 2022

Mbali na hiyo, Ne-Yo atatakiwa kumlipa mzazi mwenzake huyo Tsh. Milioni 28 kila Mwezi kwaajili ya Malezi ya Watoto wao 3, atalipa ada za Shule za Watoto pamoja na Tsh. Million 11.6 kila Mwezi kama fidia kwa Mzazi mwenzake baada ya kuachana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags