Ndoa ya kaka yake Jada Smith matatani

Ndoa ya kaka yake Jada Smith matatani

Jada Smith siyo pekee katika familia yake aliye na wakati mgumu kwenye ndoa yake, inaelezwa kuwa hadi kaka yake Caleeb Pinkett, ambaye ni muigizaji alitengana na mkewe Patricia kwa miaka mitatu na sasa Patricia amewasilisha madai ya talaka mahakamani.

Patricia aliwasilisha ombi la talaka jana Jumatatu baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka 17, kwa mujibu wa TMZ wanaeleza kuwa hati zilizopelekwa mahakamani zinaonesha Patricia na Caleeb wametengana tangu Februari 28, 2020.

Huku lengo la kwenda mahakamani ni Patricia kutaka haki ya malezi ya watoto pamoja na kulipwa fidia ya talaka. Ikumbukwe wawili hao walifunga ndoa Septemba 2006 na wana watoto miwili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags