Msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux ambae ametikisa mitandao ya kijamii Afrika kutokana na harusi yake iliyofanyika nchini Nigeria akifunga ndoa na Priscilla, na sasa tukio hilo linatajwa kupaisha muziki wake na kupenya kwenye chati za muziki nchini humo.
Jux ambaye amekuwa na ushawishi mkubwa Afrika Mashariki kupitia muziki wake na sasa upepo wake umehamia Magharibi mwa Afrika nchini Nigeria ambapo anatajwa kufanya vizuri katika chati kubwa nchini humo. huku akiwapiku mastaa wakubwa kupitia ngoma zake mbili.
Kwa mara ya kwanza Jux ameshika nafasi mbili za juu kwenye mtandao wa kusikilizia na kuuzaa muziki ‘Itunes’ nchini Nigeria kupitia ngoma zake mbili.
Jux ameshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu kwenye Jukwaa hilo nchini humo, kupitia ngoma ya God Design aliyoshirikiana na Phyno lakini pia, ngoma yake ya Ololufe Mi akiwa na Diamond Platnumz ambayo imeshika nafasi ya tatu.
Harusi ya Jux na Priscilla ambayo iliwakusanya mastaa mbalimbali wa muziki na tasnia nzima ya burudani kutoka maeneo tofauti tofauti Afrika inatajwa kuwa kichocheo kikubwa ambacho kimempaisha msanii huyo kufikia charti kubwa za muziki nchini Nigeria.

Leave a Reply