Ndege yatua kwa dharura baada ya sehemu ya ubavu kutoka

Ndege yatua kwa dharura baada ya sehemu ya ubavu kutoka

Ndege kutoka Shirika la #Alaska iliyokuwa ikisafiri kutokea Jimbo la Oregon kuelekea California nchini Marekani, siku ya Ijumaa usiku ililazimika kutua kwa dharura baada ya sehemu ya ubavu wa Ndege hiyo kunyofoka.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilitokea dakika 6 tu baada ya ndege hiyo mpya aina ya Boeing 737-9 MAX kuruka.

Ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria 171 na wafanyakazi 6 ilifanikiwa kutua salama katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Portland huku mtu mmoja tu akipelekwa hospitali kutokana na majeraha madogo.

Mamlaka ya udhibiti wa anga nchini Marekani (FAA), imeamuru kusimamishwa mara moja kwa matumizi ya ndege 171 aina ya Boeing 737-9 MAX hadi zitakapoangaliwa upya.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags