Ndege ya Urusi yaanguka kwenye makazi na kuua 13

Ndege ya Urusi yaanguka kwenye makazi na kuua 13

Watu 13 wakiwemo watoto 3 wamefariki baada ya ndege ya kivita ya Urusi kuanguka kwenye jumba la makazi katika mji wa kusini ya Yeysk, muda mfupi tu baada ya kupaa angani.

Watu wengine sita hawajulikani walipo huku 19 wakijeruhiwa. Yeysk imetenganishwa na eneo linalokaliwa na Urusi la kusini mwa Ukraine na Bahari ya Azov.

Picha za video zimeonyesha eneo la jengo hilo la ghorofa tisa likiteketea kwa moto mkubwa huku maafisa wakibaini kuwa kwa sasa moto huo umedhibitiwa.

Kamati ya Uchunguzi ya Urusi, ambayo inashughulikia masuala ya uhalifu imesema imeanzisha kesi ya jinai na kuwatuma wachunguzi kwenye eneo la tukio.

Chanzo DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags