Ndala kuamua ‘mechi’ ya Al Ahly na Simba leo

Ndala kuamua ‘mechi’ ya Al Ahly na Simba leo

Mwamuzi kutoka #DRCongo, Jean Jacques Ndala ameteuliwa kuchezesha mchezo wa mkondo wa pili wa robo fainali ya African Football League kati ya Al Ahly dhidi ya Simba SC utakaopigwa katika dimba la Cairo, Misri.

Ndala atasaidiwa na Jerson dos Santos wa Angola na Arsenio Marengula wa Msumbiji huku ‘refa’ wa akiba akiwa ni Messie Nkounkou wa Congo.

‘Refa’ Ndala amekuwa na historia nzuri na Simba ambapo katika ‘mechi’ tatu alizoichezesha, imeibuka na ushindi mara mbili na kupoteza mchezo mmoja ikiwa ni ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Jwaneng Galaxy, ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya RS Berkane na kipigo cha 2-0 dhidi ya JS Saoura.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags