Katika historia, zamani baadhi ya nchi zilikuwa na sheria kali dhidi ya mtu ‘Mmbea’ (watu waliokuwa wakisambaza na kuzungumza taarifa zisizo za kweli au zisizowahusu) walikuwa wakipokea adhabu kama vile kunyongwa ama kifungo cha maisha.
Kwa mujibu wa utafiti na historia ya sheria za kijamii na kisiasa katika maeneo nchi hizi watu walikuwa wakipatiwa adhabu kali haswa wale waliokuwa wakisambaza maneno ya umbea.
Uingereza (karne ya 16 na 17)
Wakati wa enzi ya Elizabeth I na wakati wa kifalme wa James I, watu waliokuwa wakisambaza taarifa zozote hasa kuhusu familia za kifalme, Serikali au dini na ukapatikana ushahidi wa kutosha basi watu hao waliokuwa wakishitakiwa kwa kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo cha kunyongwa.
China (zamani, kipindi cha utawala wa Qing)
Kama baadhi ya watu wanavyojua kuwa China ni moja ya nchi ambayo inasheria kali hii haikuanzia hapo kwani wakati wa utawala wa Qing inaelezwa kuwa mtu yeyote atakayezungumza taarifa za umbea na zikaleta mtafaruku kwa jamii, basi mtu huyo alikuwa akichukuliwa hatua ya kunyongwa hadi kifo katika sehemu ya wazi (hadharani) ili wengine wasirudie kitendo hicho.
Ufaransa (wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa)
Mbali na nchi hizo nchi nyingine ambayo ilikuwa na sheria kali dhidi ya watu wambea ni Ufaransa ambapo katika nchi hiyo watu hao walikuwa wakiitwa waasi hivyo hawakutakiwa kuishi kabisa na adhabu yao ilikuwa ni kunyongwa hadharani.
Watu ambao walikuwa wakijikuta katika msala huo wengi wao walikuwa ni wanawake huku wanaume wakiwa wachache zaidi tofauti na sasa kuwa wanaume ndio wanatajwa kuongoza kwa kuwa wambea. Hata hivyo sheria hizo hazipo tena
Leave a Reply