NAY WA MITEGO ajiondoa tuzo za TMA

NAY WA MITEGO ajiondoa tuzo za TMA

Msanii wa muziki wa HipHop, Emmanuel Elibarick, maarufu Nay wa Mitego, ametangaza kujiondoa kwenye tuzo za muziki Tanzania(TMA).

Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi Machi 24,2022 na Idara ya Habari na Mawasiliano kupitia ukurasa wa Instagram wa lebo yake ya FreeNation na kuthibitishwa na mwenyewe alipozungumza na Mwananchi kutaka kujua ukweli wa jambo hilo.

Nay katika tuzo hizo amechomoza katika kipengele cha msanii bora wa HipHop, akishindanishwa na wasanii wengine akiwemo Profesa J, Young Lunya, Darasa na Rapcha.

Nay amesema amelazimika kujitoa katika hizo kutokana na kukosa imani na kamati ya uchaguzi wa kazi za muziki (Academy).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags