Namna ya kutumia teknolojia kujitengenezea kazi

Namna ya kutumia teknolojia kujitengenezea kazi

Ungemuambia mtu yeyote wa zamani kama ikifika baada ya miaka kadhaa tutakuwa na uwezo wa kuwasiliana na ndugu zetu kupitia mfumo wa video, wangeweza kusema kuwa unaota, tena ndoto zisizofikika muda wowote karibuni. Hata hivyo, miaka kadhaa mbele, kwa uwepo wa tekinolojia, haya yote yamewezekana, sasa tunaweza kuishi maisha kwa urahisi Zaidi, mashine zikitufanyia kazi mbalimbali, Pamoja na kutumika kupiga mahesabu, kufua nguo, kuwasiliana na mengineyo.

Kuna umuhimu mkubwa wa kutambua namna ya kutumia tekinolojia kujitengenezea kazi mbalimbali, kwani kumekuwa na changamoto na hofu kubwa kwa watu, wakihofia kuwa tekinolojia inaweza kuja kuiba kazi za binadamu. Kama kijana, unatakiwa usiichukulie hii kama changamoto, bali kama fursa ya kuweza kujitengenezea kazi Zaidi, hasa katika kipindi hiki cha kidigitali ambapo tekinolojia nayo imepamba moto.

Leo ninakuletea mchongo wa namna ya kutumia teknolojia kujitengenezea kazi au ajira.

  1. ONLINE BUSINESSES

One of the most famous features za mitandaoni ni uwezo wa kuinteract na customers wako, Pamoja na kutangaza biashara zako. Ukiwa na social media accounts, unaweza kabisa kufanya biashara online. Tafuta angle ya kitu unachotaka kukiuza, kama ni nguo za mitumba, viatu, urembo, chakula ama hata biashara za services kama vile kujitangaza kama MC au mpambaji.

Opportunities za kufanya online business zinawezeshwa sana na technology kwani unaweza hata usimuone mteja mwenyewe, akaorder online, ukampa mtu wako wa boda akapeleka na yeye hela akakutumia kwenye simu. Technology has brought online transactions, in recent years, hela inayotumwa kupitia mitandao ya simu inazidi ile miamala ya kupitia benki. This is a great opportunity for you, vijana wengi wa chuo mna smartphones, use them to have online stores, huna haja ya kufungua duka, hapo hapo hostel panatosha!

  1. KUTENGENEZA APPLICATIONS

Another famous thing that every techy person wants to explore ni innovation. Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wanaokuja na new innovations kila siku, na wewe una opportunity ya kufanya hivyo na zaidi. Among popular innovations ni Pamoja na kutengeneza applications. These applications zinaweza kuwa ni za kwako, au ukamtengenezea mteja na kupata hela ya maana tu.

Kujifunza skills kama coding, UI na UX vinaweza kukusaidia sana kujiajiri hata ukiwa hapo hapo ulipo, tena uzuri zaidi ni kwamba hauna hata haja ya kwenda ofisini, you can do it as a freelancing gig, na kujipatia pesa ndefu.

Applications kama za Mtabeapp, Soka app, eGazeti, zote zimetengenezwa na vijana kama wewe, sasa wewe unashindwa nini? Chakalikaaa.

  1. UBER, BOLT AND AIRBNB

Kama na hii ulikuwa hauijui basi upo nyuma sana! Dunia imebadilika sana siku hizi. Wenye Uber hawana magari, wenye AirBnB hawana nyumba ila biashara zao zinaenda. Kama unagari lako si bora uregister kwa Uber au Bolt au hata zote kwa pamoja na uanze kukusanya pesa zako.

Uber na Bolt zitakusaidia kuendesha biashara yako kwa kuendesha watu kutoka sehemu moja hadi nyingine pale watakapo kurequest.

Lakini pia unaweza ukawa hauna gari, ila unapa kukaa, au umepanga, unaweza pia kuilist hiyo sehemu katika AirBnB na ukapangisha either hiyo nyumba au hata chumba kimoja tu, kila mteja atakapotaka kulala hapo atakulipa kulingana na bei uliyoiweka.

Technology kwa kweli imeleta mabadiliko makubwa sana, before ungekaa na kuwaza ufanya nini, ila kwa sasa mambo mengi ni kitonga tu, ni wewe kuchangamkia furs ana kuona kutokana na vitu nilivyonavyo, ni vitu vipi naweza kuvifanya vikaniingizia kipato?

  1. UWAKALA

Nani hajatumia TigoPesa, MPesa au Airtel Money? Ukweli ni kwamba hii ndio habari ya mjini! Njia mpya ya kutuma, kutoa na kuweka pesa ni kupitia simu, na hapo ndipo unapopata upenyo wa kufanya hii kuwa fursa kwako!

Unaweza ukajifungulia biashara ya uwakala na ukawa unaweka na kutoa pesa za watu una kupata commission yako. Kama unaweza kujikusanyia kiasi Fulani cha mtaji wa kuanzia, hii ni biashara nzuri sana, hasa ukiwa maeneo ya chuoni, kwani huko ndiko kuna mzunguko wa pes ana uwingi wa watu.

Hizi ni baadhi tu ya mifano ambayo unaweza kutumia teknolojia kujitengenezea kipato. Changamka kijana, na opportunities zilizopo, utaweza kutoboa one way or the other! Use technology kujisogeza mbele kwani possibilities with tech are endless!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags