Namna Ya Kutengeneza Chesee Balls

Namna Ya Kutengeneza Chesee Balls

Wakati waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa  wamemaliza mfungo na kula Eid, waumini wa Kikristo bado wanaendelea na mfungo. Hivyo tumewasogezea jinsi ya kutengeneza kitafunwa ambacho wanaweza kukitumia wakati wa kufturu.

Cheese ball ni aina ya vitafunwa vinavyotengenezwa kwa kutumia jibini, mara nyingi huongezwa viungo kama tambi nyembamba kwa ajili ya kuongeza ladha zaidi. Kitafunwa hicho hutumika zaidi hasa kwenye matukio ya mkusanyiko wa watu ama sherehe.

Cheese ball ni kitafunwa chenye asili ya Marekani na Uingereza ingawa ni maarufu katika maeneo mengi duniani. Inakisiwa kuwa ilianza kuwa maarufu katika karne ya 20 kutokana na urahisi wake katika utengenezaji wake.

 

MAHITAJI

  1. Ngano robo
  2. Tambi nyembambe kiasi (utazipata Super Market)
  3. Triangle chesee vipande vinne (pia zinauzwa Super Market)
  4. Sukari vijiko viwili vya chakula
  5. Hamira kijiko kimoja
  6. Mafuta ya kukandia ngano kijiko kimoja cha chakula
  7. Vanila kijiko kimoja
  8. Maziwa kikombe kimoja (yawe ya uvugu vugu).
  9. Sweetened Condensed Milk

 

 

NAMNA YA KUANDAA/KUPIKA

  1. Chukua maziwa yako ya uvugu vugu kisha uweke hamira pamoja na sukari.
  2. Baada ya hapo koroga kidogo mchanganyiko wako na kisha utauacha kidogo kwa dakika 5-10
  3. Huku ukiwa unasubiri mchanganyiko wako utachukua Triangle Chesee zako na utaaza kuzikata vipande vidogo vidogo kisha utaweka kwenye friza ili zipate baridi.
  4. Utachukua mchanganyiko wako kisha utaweka unga wako wa ngano, mafuta ya kula kijiko kimoja pamoja na vanila.
  5. Anza kukanda ngano yako mpaka pale itakapo kuwa imelainika kabisa.
  6. Halafu utaanza kukata madonge madogo madogo mpaka umalize. Ukishamaliza utatoa chesee yako kwenye friji.
  7. Baada ya hapo chukua donge moja moja na uweke chesee katikati ya donge la ngano hakikisha unafunga ndonge lako ili mafuta yasije kuingia ndani ya chesee.
  8. Baada ya kumaliza kufanya hivyo katika madonge yako yote ya ngano utayaacha kwa dakika 10 yaweze kuumu. Utachukua tambi zako nyembamba utazikata ndogo ndogo kiasi utaziweka kwenye sahani .
  9. Chesee balls zikiumuka utachukua moja moja utachovya kwenye bakuli la maziwa kisha utazimwagia tambi pande zote.
  10. Utafanya hivyo mpaka utakapomaliza zote kisha utabandika kalai jikoni utatia mafuta yatakapopata moto utaanza kukaanga mpaka utakapomaliza zote. Ukimaliza utazimwagia Sweetened Condensed Milk yako.

Na mpaka kufikia hapo kitafunwa chako kitakuwa tayari na unaweza kula na Juice, chai, kahawa na hata soda. Vile vile unaweza kutumia kama biashara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags