Nabi kurudi siku ya wananchi

Nabi kurudi siku ya wananchi

Aliekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga Nasreddine Nabi amefichua kwamba Bilionea Ghalib Said Mohamed 'GSM' amempa mualiko rasmi kwamba atafurahi kumuona kwenye Tamasha la kilele cha Wiki ya Wananchi cha msimu huu.

Nabi alisema endapo atakuwa hana ratiba ngumu atarudi haraka kuja kufungana na familia yake kwa kuwa Yanga ni watu wake alioishi nao kwa furaha.

"Nilipokwenda kumuaga bwana Ghalib aliumia, nami niliumia sana, unajua Ghalib alinipa heshima kubwa sana wakati wote niko hapa nilikuwa sehemu ya familia yake kama ambavyo anaishi na ndugu zake, amenialika nije kwenye kilele cha wiki ya wananchi na kuhakikishia kama sitakuwa na ratiba ngumu yoyote nitarudi hapa kuja kuungana na familia hii," alisema Nabi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags