Mzee Yusuph, Nataka kumuoa Didah

Mzee Yusuph, Nataka kumuoa Didah

Alooooooo! Nyie nyie nyie kuna watu wanabahati haswaa wakati wengine wa kugombewa kuolewa wewe utaendelea kufa single, sasa bwana  zilizokiki hivi punde  kutoka kwa yule msanii mkongwe katika muziki wa Taarabu Mzee yusuph baada ya kufunguka kuwa anatarajia kufunga ndoa na mtangazaji wa kipindi cha mashamsha Didah Shaibu.

Mzee Yusuph ameyasema hayo katika mahojiano yake na chombo kimoja cha habari nchini na kueleza kuwa “nampenda Didah na natarajia kufunga nae ndoa, wote walio pita nae hawamuwezei mimi ndo namuwezea” amesema Mzee Yusuph

Aidha Mzee Yusuph aliendelea kufunguka kuhusiana nayeye na aliekuwa mume wa Didah nani wa kwanza alieleza kuwa “ aliekuwa mume wa Didah Omary Kumbilamoto aliingilia mapenzi yetu, baada ya kuachana nae sasa huu ni muda muafaka wa mimi kumuoa” amesema Mzee Yusuph






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags