Mwigizaji wa Super size me afariki dunia

Mwigizaji wa Super size me afariki dunia

Mwandishi wa filamu na mwigizaji kutoka Marekani Morgan Spurlock, ambaye alijulikana zaidi kupitia filamu yake ya mwaka 2004 iitwayo ‘Super Size Me’ amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 53 baada ya kusumbuliwa na saratani kwa muda mrefu.

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na familia yake huku kaka yake Craig Spurlock kupitia ukurasa wake wa Instagram alitoa salamu zake za mwisho kwa ndugu yake kwa kueleza kuwa Morgan alikuwa bado ana mengi ya kuinua Sanaa, hivyo dunia itambue imepoteza mtu wa muhimu sana.

Morgan Spurlock amewahi kuongoza na kuonekana katika filamu kama ‘POM Wonderful Presents’, ‘One Direction: This Is Us’, ‘Mansome’, ‘Cave-O-nomics’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags