Mwigizaji Saif Ali Khan Achomwa Kisu

Mwigizaji Saif Ali Khan Achomwa Kisu

Mwigizaji nguli wa Bollywood kutoka India Saif Ali Khan ameripotiwa kufanyiwa upasuaji wa dharura katika Hospitali ya Lilavati jijini Mumbai baada ya kuchomwa kisu na jambazi aliyevamia makazi yake yaliyopo Bandra.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali tukio hilo limedaiwa kutokea mapema leo Alhamisi Januari 16, 2025 ambapo Saif alimkuta mvamizi huyo ndani ya ghorofa yake ya 11 akiwa anazozana na mfanyakazi wa nyumbani kwake ndipo akaamua kuuingilia ugomvi huo jambo ambalo lilipekelea kuchomwa visu sehemu tofauti ikiwemo na maeneo ya uti wa mgongo.

"Imebainika kuwa mtuhumiwa alitumia ngazi ya dharura kuingia ndani ya nyumba yao. Hadi sasa, uchunguzi unaonyesha kwamba ilikuwa jaribio la wizi. Tunafanya kila jitihada kumkamata mtuhumiwa haraka iwezekanavyo. Akishakamatwa, tutaweza kufichua maelezo zaidi." DCP Dixit Gedam ametoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari

Khan, ambaye ni mkongwe wa tasnia ya filamu ya India kwa zaidi ya miongo mitatu, ametoka katika moja ya familia maarufu zaidi Bollywood akiwa kama mtoto wa nyota wa kriketi Mansoor Ali Khan Pataudi na mwigizaji Sharmila Tagore.

Alionekana katika televisheni kwa mara ya kwanza mwaka 1993 kupitia filamu ya Parampara na alianza kujulikana na kupata mafanikio kupitia filamu za mwaka 1994 Yeh Dillagi, Main Khiladi Tu Anari na filamu nyingine kama Dil Chahta Hai (2001), Kal Ho Naa Ho (2003), Hum Tum (2004) na nyinginezo.

Kwa sasa mwigizaji huyo amefunga ndoa na mwigizaji mwenzake kutoka Bollywood Kareena Kapoor Khan ambapo wamejaaliwa kupata watoto wawili ambao ni Taimur (8) na Jeh (4).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags