Mwigizaji Ray Liotta Afariki dunia

Mwigizaji Ray Liotta Afariki dunia

Aisee moja kati ya taarifa ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ni hii hapa inayohusiana na kifo cha mwigizaji Mashuhuri duniani Ray Liotta .

Ray Liotta amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 67. Ambapo kifo chake kinasemekana kuwa  amefariki akiwa usingizini katika Jamhuri ya Dominika ambapo alikuwa akifanya filamu mpya ya “Dangerous Waters” kisiwani humo.

Aidha taarifa zinaeleza kuwa hapakuwa na chochote cha kutiliwa shaka kuhusu kifo hicho. Mchumba wake Ray Jacy Nittolo alikuwa naye huko Dominican Republic alipokuwa akifanya kazi kwenye filamu hio.

Nikukumbushe tu kwamba wengi tulimuona Ray kwenye kazi zake bora zaidi kama The Good Fellas, akiwa na Robert De Niro na Joe Pesci na hivi karibuni tulimuona kwenye show ya tv ya kipolisi ya ‘Shades Of Blue’ akiwa na J LO.

Hata hivyo Ray ameacha mtoto mmoja wa kike, Karsen Liotta, ambaye pia ni muigizaji.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags