Mwigizaji Bill Cobbs afariki dunia

Mwigizaji Bill Cobbs afariki dunia

Mwigizaji mkongwe wa Marekani Bill Cobbs ambaye amejulikana zaidi kupitia filamu zake kama ‘Night at the Museum’ na ‘The Bodyguard’ amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.

Taarifa ya kifo chake ilithibitishwa na mmoja wa mwanamfamilia wa Cobbs katika mtandao wa Facebook siku ya jana Jumatano, kwa kueleza kwamba mwigizaji huyo amefariki dunia June 25 kwa Amani nyumbani kwake New York City, Marekani.

Muigizaji huyo, ambaye alifanya kazi kwa miaka minane kama fundi rada wa Jeshi la Anga kabla ya umaarufu wake alizaliwa Cleveland, Ohio na kuhamia New York City mwaka 1970 akiwa na umri wa miaka 36, huku filamu yake ya kwanza ikiwa ‘The Taking of Pelham One Two Three’ ya mwaka 1974.

Cobbs alijulikana zaidi kupitia filamu mbalimbali alizozicheza ikiwemo ‘Air Bud’, ‘Demolition Man’, ‘The People Under the Stairs’ na nyinginezo. Mwaka 2020 alipata tuzo ya ‘Emmy’ katika uhusika wake kwenye animation ya ‘Dino Dana’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags