Mwenye sherehe alivyotaka waalikwa wawe na urefu sana

Mwenye sherehe alivyotaka waalikwa wawe na urefu sana

Kawaida linapokuja suala la kufanya sherehe ya aina yoyote, muhusika ndiyo huamua anataka iwaje. Kwa upande wa Hans Hemmert mwaka 1997 aliamua kutengeneza viatu vyenye visigino ili wageni waalikwa waweze kulingana urefu.

Hans aliandaa sherehe hiyo kama sehemu ya maonesho yake ya ‘Personal Absurdities’ yaliyofanyika Galerie Gebauer huko Berlin, wakati wa kuandaa moja ya kitu ambacho alifikiria ni kuondoa ubaguzi wa watu warefu na wafupi.

Ndipo aliwataka wageni waalikwa kulingana urefu kwa kutengeneza viatu vyenye visigino vya aina tofauti vitakavyowawezesha kuwa na urefu sawa ili watakapozungumza waweze kutazamana usoni.

Hemmert wakati wa mahojiano yake kwenye sherehe hiyo alifunguka kuwa alifanya hivyo ili kuondoa ubaguzi wa watu wafupi na warefu huku lengo kuu likiwa ni kila mmoja kujiona sawa kwa mwenzake.

Aidha kwa mujibu wa baadhi ya tovuti zinaeleza kuwa kila mgeni alipaswa kuwa na urefu wa futi 6 na inchi 6 (mita 2) hivyo basi ambaye angakuwa chini ya hapo angepewa viatu hivyo ili aweze kuwafikia wenzake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post