Mwenye miaka 80 ashiriki Miss Universe

Mwenye miaka 80 ashiriki Miss Universe

Mwanamitindo kutoka Korea Choi Soon-hwa mwenye miaka 80 ameripotiwa kushiriki katika mashindano ya Miss Universe 2024, huku akitajwa kuwa mshiriki mwenye umri mkubwa zaidi katika mashindano hayo.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali bibi huyo wa wajukuu watatu ametajwa kuwa mmoja wa washiriki 32 wanaowania taji hilo kugombania nafasi ya kuiwakilisha Korea mwezi Novemba mwaka huu.

Choi ameingia kwenye mashindano hayo baada ya kuondolewa kwa sharti la ukomo wa umri pamoja na la kuwa mzazi (mtu mwenye mtoto), ambapo anakuwa mshiriki wa pili mwenye umri mkubwa kwa mwaka 2024, mwingine ni kutokea Singapore akiwa na umri wa miaka 62, huku mshindi wa kwanza nchini humo akiwa ni mama wa mtoto mmoja.

Ndoto ya Choi kutaka kuwa mwanamitindo ilianza akiwa kwenye kituo cha kulea wazee mwaka 2014, baada ya mmoja wa wazee kumwambia anaweza kufanya vizuri katika mambo ya mitindo ndipo akiwa na miaka 71 alianza shule kujifunza mambo hayo.

Miaka minne baadaye 2018, akiwa na miaka 75 alianza rasmi kazi za mitindo na alitembea katika maonyesho ya mavazi ya wiki ya Fashion huko Seoul, na toka muda huo ameweza kutokea katika majarida mbalimbali kama Harper Bazaar na Elle.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags