Mwendokasi Mbagala kuanza leo

Mwendokasi Mbagala kuanza leo

Safari za magari yaendayo kasi maarufu kama (Mwendokasi) kutoka Gerezani hadi Mbagala zinaanza rasmi leo kuelekea msimu wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 (Sabasaba) ambapo jumla ya magari 30 yataanza kutoa huduma.

Safari hizo zinazoanza leo ambapo gharama ya nauli ni Tsh.750 kwa tiketi ambazo pia zitatolewa kwa njia ya mtandao kupitia application ya DART.

Akiongea wakati wa kuzindua safari hiyo Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), Deusdedit Casmir amesema wataongeza watumiaji wa magari hayo kwa asilimia 50 ambapo pia wataanza na magari 20 kwa siku ya leo na kuendelea kuongeza.

Aidha katika safari hiyo inayoanzia Kariakoo Gerezani hadi kituo kikuu cha Mabagala (Terminal) vitatumika pia vituo vinne vya Kati ambavyo ni Sabasaba, Mission, Zakhem na Mbagala Rangi tatu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags