Waandishi wa habari katika kituo cha habari kikongwe nchini Kenya cha Citizen Tv wanaripotiwa kulishwa sumu baada ya kula chakula siku ya Boxing day, wafanyakazi hao walianza kulalamika kuumwa na tumbo ndipo wakakimbizwa hospitali.
Hii ni baada ya kula chakula kilichoandaliwa na kampuni maarufu ya upishi, kituo hicho cha habari kiliwaomba wapishi hao wawandalie chakula wafanyakazi wao wanaofanya kazi katika siku ya sikukuu.
Hii imepelekea kumpoteza mwandishi wa habari mmoja ambae hakutajwa jina lake mpaka hivi sasa.
Kampuni ya habari ya Royal Media Services (RMS) imethibitisha taarifa hiyo kwa kutoa ujumbe uliokuwa unasema “Royal Media Services (RMS) ina huzuni kuthibitisha kisa kibaya cha sumu ya chakula ambacho kiliathiri idadi kubwa ya wafanyikazi wanaofanya kazi wakati wa zamu ya Krismasi”
“Kwa kuzingatia mipango ya kazi ya kipindi cha likizo, RMS ilishirikisha kampuni ya kibinafsi ya upishi wa chakula ili kutoa milo kwa wafanyikazi wanaofanya kazi wakati wa zamu ya Krismasi”
“Siku ya Boxing Day Desemba 26, 2022, baadhi ya wafanyakazi walilalamika kuhusu maumivu makali ya tumbo baada ya kula milo inayotolewa ndani ya majengo ya kampuni”
“Tumeshtushwa na kuhuzunishwa sana kuujulisha umma kuwa mtumishi mmoja amefariki kwa bahati mbaya kutokana na ugonjwa huo unaodhaniwa kuwa ni sumu kwenye chakula. Mawazo na maombi yetu yapo pamoja na familia ya mfanyakazi wetu aliyefariki katika kipindi hiki kigumu”
“Wafanyikazi kadhaa pia wamelazwa hospitalini kwa tuhuma za sumu, RMS inatoa usaidizi wote unaohitajika kwa wafanyikazi walioathiriwa na tukio linaloshukiwa la sumu ya chakula kwa sasa linachunguzwa”
Wachira Waruru
MKURUGENZI MSIMAMIZI WA KUNDI
Leave a Reply