Mwanaume aliyepandikizwa uso baada ya ajali apata mpenzi

Mwanaume aliyepandikizwa uso baada ya ajali apata mpenzi

Mwanaume kutoka New Jersey anayefahamika kwa jina la Joe Dimeo, ambaye alipata ajali ya gari mwaka 2018 baada ya kusinzia akiwa anaendesha na kisha kufanyiwa upandikizaji wa uso na mikono hatimaye apata mpenzi.

Ajali hiyo aliipata baada ya kusinzia wakati akiendesha na kusababisha gari kupinduka na kuteketea kwa moto, jambo lililofanya apate majeraha asilimia 80 ya mwili wake, kama madaktari walivyodai.

Baada ya ajali hiyo mwanaume huyo alitakiwa kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya upandikizi wa sura mpya na mikono, kutokana na msaada wa madaktari alifanikiwa kupandikizwa sura mpya tofauti ya yake ya awali.

Hata hivyo pamoja na changamoto zote Joe amedai kuwa ajali hiyo haijamfanya tu kupata uso na mikono mipya bali imemfanya aweze kupata mwenza mwenye upendo wa dhati ambaye anafahamika kama Jessica Koby.

Inaelezwa kuwa mwanadada huyo baada ya kusikia taarifa za ajali mwaka 2018 aliguswa na tatizo alilopata Joe na ndipo alimtafuta na kuanza ukaribu wa kumuhudumia tangu akiwa mgonjwa hadi alipopona mwaka 2020 na sasa wameamua kuwa wapenzi.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post