Mwanasheria wa Diddy afunguka chupa 1,000 za mafuta

Mwanasheria wa Diddy afunguka chupa 1,000 za mafuta

Ikiwa zimetimia siku 11 tangu mkali wa Hip hop Marekani, Sean Combs 'Diddy' ashikiliwe na polisi kwa makosa matatu, mojawapo likiwa la biashara ya ngono, hatimaye mwanasheria wake, Marc Agnifilo, amefunguka madai ya serikali kukamata chupa 1,000 za mafuta ya watoto na vilainisha nyumbani kwa rapa huyo.

Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ jana Jumatano Septemba 25, 2024 ilichapisha ripoti kuhusu filamu ya Combs iitwayo ‘The Downfall of Diddy: The Indictment.’

Ambapo ndani ya filamu hiyo wakili wa Combs alizungumzia chupa za mafuta zilizokamatwa na maajenti wa shirikisho nyumbani kwa Diddy Machi huku akieleza kuwa haamini wingi wa chupa hizo.

“Sijui ni wapi hizo chupa 1,000 zilipotokea, siwezi kufikilia kabisa kwa sababu chupa moja ya mafuta unaweza kuitumia kwa muda mrefu, hata hivyo mafuta ya watoto yanahusiana vipi na jambo lolote, yaani ana nyumba kubwa na hununua vitu kwa wingi.

"Nafikiri wana maduka (Costco) kila mahali, kwenye nyumba zake na anaponunua nyumba sehemu yoyote ile, hebu tuseme tu zilikuwa nyingi, sawa lakini haziwezi kufika 1,000,” amesema Marc

Utakumbuka kuwa nyumba za Diddy zilizopo Los Angeles na Miami zilipigwa msako na mamlaka ya usalama wa Taifa kufuatia tuhuma za unyanyasaji wa kingono zilizokuwa zikimkabili toka mwaka jana.

Siku moja baada ya kukamatwa kwake Septemba 17, 2024 mamlaka zilifichua kuwa wakati wa msako nyumbani kwa Diddy walikuta vitu kama dawa za kulevya, zaidi ya chupa 1,000 za mafuta ya watoto na vilainishi na bunduki tatu za AR-15 zenye nambari za usajiri usio wake.

Kwa sasa Diddy anashikiliwa kwenye gereza lenye historia ya mauaji nchini Marekani la ‘The Metropolitan Detention Center (MDC) ambapo atakuwa hapo hadi pale kesi yake itakapoanza kusikilizwa.

Documentary ya Diddy iliyopewa jina la ‘The Downfall of Diddy: The Indictment inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni kupitia mitandao ya kuangalia filamu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags