Mwanariadha Kipruto afungiwa miaka sita

Mwanariadha Kipruto afungiwa miaka sita

Anayeshikiria rekodi ya dunia ya mbio za barabarani za kilomita 10 na mshindi wa medali ya shaba ya Dunia ya mita 10,000 ya mwaka 2019 Rhonex Kipruto kutoka Kenya amepigwa marufuku kwa miaka sita kushiriki mchezo wa riadha.

Marufuku hiyo imetolewa na kitengo cha Uadilifu cha Riadha (AIU) baada ya kuripotiwa kutumia dawa za kusisimua misuli huku Mahakama ya kinidhamu ikigundua dosari katika pasipoti ya Kibailojia ya Kipruto (ABP) ambapo atatumikia kifungo hicho hadi 2029.

Aidha kwa mujibu wa AIU imeweka wazi kuwa Kipruto mwenye miaka 24 atapoteza rekodi yake ya dunia ya mbio aliyoiweka mwaka 2020 jijini Valencia pamoja na medali ya shaba ya ubingwa wa dunia aliyoshinda nchini Qatar.

Licha ya Kipruto kukanusha mashitaka, jopo hilo lilihitimisha kuwa alihusika katika na kitendo hicho.

AIU ilifanya majaribio zaidi ya wanariadha 4,700 mwaka 2023 huku ikiahidi kuwa itaendelea na mpango.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post