Mwanamuziki na producer maarufu Marekani, Roy Ayers amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa na familia ya nguli huyo katika muziki wa Soul na Jazz kupitia tovuti ya Variety inaeleza kuwa alifariki dunia Machi 4, 2025 huku ugonjwa uliokuwa ukimsumbua haukuwekwa wazi.
Katika maisha yake ya muziki, Ayers alijitambulisha kama mwanzilishi wa jazz-funk na alikuwa na mchango mkubwa katika harakati ya neo-soul.Kama msanii wa kujitegemea, alitoa albamu nyingi tangu mwaka 1963, na akapata mafanikio makubwa kupitia wimbo wake wa “Everybody Loves the Sunshine” akiwa na kundi lake la Roy Ayers Ubiquity.
Nyimbo zake zimesampuliwa na wasanii mbalimbali, akiwemo Mary J. Blige, Common, Tyler, the Creator, hadi Kanye West. Aidha, alishirikiana na wanamuziki mashuhuri kama The Roots, Guru, Fela Kuti, na Rick James.

Leave a Reply