Mwanamuziki George Strait avunja rekodi

Mwanamuziki George Strait avunja rekodi

Mwanamuziki wa Marekani George Strait amevunja rekodi nyingine katika taaluma yake ya muziki kwa kuujaza uwanja na kuifanya show yake hiyo kuweka historia mpya ya mauzo ya ‘tiketi’.

Kwa mujibu wa tovuti ya Billboard mzaliwa huyo wa Texas aliweka rekodi mpya kwa kuingiza mashabiki 110,905 katika show yake iliyofanyika kwenye uwanja wa Kyle wa Texas A&M.

Rekodi hiyo iliipiku rekodi ya awali iliyokuwa ikishikiriwa na Grateful Dead, ambaye alijaza mashabiki na kuuza ‘tiketi’ 107,019 katika show yake ya mwaka 1977 kwenye Raceway Park huko Englishtown, N.J.

Wakati tamasha la Strait likiweka rekodi mpya kwa matukio yaliyokatiwa ‘tiketi’, tamasha jingine ambalo liliwahi kupata mashabiki wengi ni tamasha la bure la mwaka 1986 lililofanyika New York Philharmonic katika ukumbi wa Central Park, ambalo lilipata takribani watu 800,000.

Mwanamuziki na mwigizaji George Strait anatamba na ngoma zake kama ‘Amarillo by Morning’, ‘Write This Down’, ‘Run’ huku akionekana katika filamu kama ‘The Soldier’, ‘Grand Champion’, ‘Pure Country’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags