Mwanamuziki dayoo aeleza kupotezana na baba yake, Safari ya kumtafuta, Ugumu wa maisha, Mafanikio ya muziki wake

Mwanamuziki dayoo aeleza kupotezana na baba yake, Safari ya kumtafuta, Ugumu wa maisha, Mafanikio ya muziki wake

Nisikuchoshe wala nisijichoshe burudani imepata waburudishaji na waburudikaji, week hii tupo na Mangi haha ukisikia naitwa “Mangiii yani Chaga tenaa”, kichwani kwako anakuja msanii gani? haya niwasanidie tu , tupo na Dayoo mkali huyu wa muziki wa Bongo Fleva, akitupa exclusive kibao.

Tunafahamu kuwa siku za hivi karibuni baadhi ya ma- star wamekuwa wakiwakataa wazazi wao ambao wamejiokeza ukubwani baada ya msanii kupata jina, let me tell you this kwa upande wa Dayoo alielewa uchungu wa baba hadi kuamua kufunga safari kuelekea Kenya kumtafuta mshua wake.

Kwenye mahojiano ambayo Mwananchi Scoop tumefanya na Dayoo ametueleza kuwa alikuwa katika malezi ambayo hakukuzwa na baba yake baada ya wazazi wake kutengana na kupelekea maisha magumu ya Dayoo na mama yake kulala nje huku chakula kikiwa mtihani.

Dayoo ametueleza ilifika wakati mama yake alimbidi kuiba mihogo kwenye mashamba ya watu ili tu aweze kupata chakula kwa ajili yake na mwanaye, huku kipindi chote hicho baba yake akiwa hatambuliki sehemu alipo.

Si tunaelewa tena baadhi ya wazazi wakitengana basi yule aliye karibu na mtoto hupenda kupandikiza chuku kwa mtoto dhidi ya mzazi mwenziye but kwa upande wa mama yake Dayoo wala haikuwa hivyo kwani mama yake ndiye alikuwa mmoja wa kumsaidia nauli na kumpa maelekezo Mangi ili akaonane na baba yake japo safari yake haikuzaa matunda kwani hakumpata baba yake Mkoani Kilimanjaro baada ya kukuta mzee wake kahamia nchini Kenya kutafuta maisha.

Dayoo ametupitisha katika safari yake hii yenye kujifunza mengi , kumkosa baba yake haikuwa sababu ya kutoonana naye kwani alifunga safari hadi nchini Kenya ambako ndiko alifanikiwa kuonana na baba yake, kwa hilo tumpe Dayoo maua  yake kwani anatuambia ugomvi wa wazazi mtoto haumuhusu ndiyo maana hakusita kumtafuta mshua wake.

Safari ya muziki wake nayo tuliigusa kwa undani kabisa tukataka kujua Mangi anajiamini nini kwani wasanii wengine wanaendelea kutikisa Speaker na Amapiano lakini kwa upande wake ndo kwanza katoa zawadi ya “Nana” ngoma yenye miondoko fulani hivi ya kupoa, sasa basi Mangi anatuambia anajiamini na muziki wake pia “Nana” ni maalimu kwa ajili ya kuwapumzisha watu baada ya kuruka na Amapiano.

Basi bwana Dayoo si akatuvujishia siri kuwa yupo single yani hana mchuchu  tangu atoe ngoma yake ya kwanza, mmhhhh mimi ilinibidi niamini tu lakini kaa ukijua jimbo lipo wazi mkali yuko Singleeee.

 

Anaeleza kuwa muziki wake umempatia maendeleo makubwa kwani ameweza kumbadilishia mama yake biashara ya mwanzo ambayo alikuwa akiuza pombe lakini kwa sasa kampatia mtaji wa kufanya biashara nyingine, akatudokezea pia kuwa ili aweze kupeform kwenye tamasha lako basi lazima umlipe kuanzia milioni tatu, hahaha faaa utani kwa Mangi na hela wewe.

All in all pongezi ziende kwa Mangi kwani kwa aliyotupitisha kwenye historia ya maisha yake yanafunzo kubwa kwa jamii hasa katika malezi ya watoto, so i hope you learn something kutoka kwa Dayoo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags