Mwanamke usimwambie mwenza wako mambo haya

Mwanamke usimwambie mwenza wako mambo haya

Ebwana mambo vipi? Msomaji na mfuatiliaji wa jarida la Mwananchi scoop hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini ukiwa kwenye mahusiano ya ndoa hutakiwi kumwambia kila kitu mwenza wako?

Je unafahamu kwanini hutakiwi kumueleza kila kitu na hasa ni mambo yapi ambayo hayafai kumueleza mwenza wako, fuatilia dondoo hii ili uweze kujiimarisha Zaidi katika masuala ya mahusiano ili yasijekuvunjika.

Bila shaka haipaswi kuwa siri baina ya wanandoa, lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo mwanamke hapaswi kumwambia mume wake, hata kama wanapendana kiasi gani.

Twende sawa haya hapa mambo ambayo mwanamke hapaswi kumwambia mwenza wake.

  1. Idadi ya wanaume uliojamiiana nao kabla ya kuoana na mume wako

Hupaswi kumfahamisha mpenzi wako wa kiume au mume wako ni wanaume wangapi ulikutana nao kimwili kabla ya kuishi naye.

Sababu ni kwamba unaweza kufikiri hautamkosea mume wako siku sijazo. Na kama idadi ya wanaume uliyomwambia ni wengi anaweza kufikiri wewe ni kahaba au mzinzi.

Kwahiyo, iwapo atakuuliza ni wanaume wangapi ulishawahi kukutana nao kimwili, unaweza kucheka tu na umwambie: ''Ebu acha, tuachane na hayo, lakini suala la ni wangapi halihusiani na safari ya mapenzi. ".

  1. Kusema siri za mpenzi wako wa kiume au mume wako wakati mmoja

Ukiulizwa maswali kumuhusu mwanaume, mjibu machache

Usiseme mambo ambayo yanaweza kumfanya mume au mpenzi wako ahisi kwamba sio bora, au ajihisi kuwa mtu mbaya

Usizungumzie kuhusu -ungependa kuwa na uhusiano na mwanaume tajiri kiasi fulani, mwenye uwezo wa kingono kiasi gani, na ni kwa vipi ungependa ampende mke wake..

  1. Usimwambie mume wako kwamba unampenda sana rafiki yako au shemeji yako

Sote tunafahamu kuwa inawezekana kwa rafiki au shemeji kutaka kukuoa.

Lakini, ni hatari kumwambia mume wako kuhusu wazo hili .

Sababu ni kwamba mume wako anaweza kuanza kuwa na mashaka kuhusu tabia zake na vitendo vyako kumuhusu mwanaume huyo, jambo linaloweza kusambaratisha ndoa yako.

  1. Usijaribu kumwambia kuwa unamchukia mama yake au familia yake

Hata mama mkwe awe ni mtu mbaya kiasi gani, usimwambie mume wako kuwa unamchukia.

Au unaichukia familia yake. Hata kama umekasirika kiasi gani, usijaribu kusema mambo mabaya kuwahusu, au kumuona mume wako sawa na familia yake. .

Kama haupatani na yeyote katika familia ya mume wako, elezea kwa utulivu, ukiwa na matumaini kuwa ataelewa ni kwanini haupatani nao.

Mume wako pia ataweza kukusaidia kutatua tatizo, na pia itazuwia matatizo mengine ambayo yanaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi.

  1. Usimtishe mume wako kuwa utakuja kuachana naye

Siku utakapomwambia mume wako kuwa utaachana naye wakati mnazozana, jua ndio mwanzo wa malumbano ndani ya ndoa.

Ndoa itaanza kukumbwa na misukosuko, wasi wasi na kutoaminiana.

Kutishia kutoa talaka katika ndoa inamaanisha kuwa hauna moyo wa imani katika ndoa, na hauoni umuhimu wake.

Isipokuwa kama katika ndoa kuna unyanyasaji au uhalifu mwingine mbaya, ni vyema kujaribu kushirikiana kutatua changamoto zozote mlizonazo.

Mwanachi scoop tumekuekea hayo machache kama kuna mengine ambayo unayafahamu unweza kutuambia kwa kudondosha comment yako hapo chini ahsanteee!!

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post