Mwanamke mwenye ndevu ndefu duniani

Mwanamke mwenye ndevu ndefu duniani

Na Aisha Lungato

Mambo vipi! Jumanne kama ya leo tunakuletea yale mambo ya kushangaza dunia leo nakuletea mwanadada Harnaam Kaur mwenyew umri wa miaka 24, ambaye ni mwanamke kutoka huko Slough, Berkshire nchini Uingereza aliyeshikiria rekodi ya mwanamke wa kunza kuwa na ndevu ndefu duniani.

Harnaam amesema ni heshima kubwa kwake kutambuliwa kuwa mwanamke anayeishikiria rekodi ya dunia nzima pia ameeleza kuwa ndevu hizo ndefu ni kama sehemu ya juhudi zake za kukabiliana na watu wengi waliomkejeli kutokana na muonekano wake.

Kwa mujibu wa madaktari wameeleza kuwa, Bi Kaur ana tatizo la homoni lifahamikalo kwa Kiingereza kama polycystic ovary syndrome, ambalo humfanya mwanamke kuwa na nywele zaidi kuliko kawaida usoni.

Machi 2016 Harnaam Kaur alikuwa mwanamke wa kwanza kushiriki maonyesho ya mitindo ya London Fashion Week akiwa na ndevu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags