Mwanamke aliyefariki azinduka wakati wa kuzikwa

Mwanamke aliyefariki azinduka wakati wa kuzikwa

Baadhi ya raia wa Ecuador wameachwa na mshangao baada ya mwanamke aliyetambulika kwa jina la Bella Montoya mwenye umri wa miaka 76 kukutwa akihangaika kuvuta pumzi kwenye jeneza wakati ndugu walipotaka kumvalisha mavazi maalumu ya mazishi.

Taarifa ya wizara ya afya inasema, Bella alipata tatizo la mshtuko wa moyo uliotokana na kushindwa kupumua vizuri, na hata alipofanyiwa huduma ya kushtuliwa mapigo ya moyo hakuweza kuamka na hivyo kutangazwa kuwa amefariki.

Mwanamke huyo baada ya kuzinduka alirudishwa hospitali na kuwekwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU) huku timu ya madaktari ikifanya uchunguzi zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags