Mwanamitindo Nada afunga ndoa na bilionea wa PTL

Mwanamitindo Nada afunga ndoa na bilionea wa PTL

Mkurugenzi kampuni inayojihusisha na mitindo ya nguo za wanawake Pretty Little Thing (PLT), bilionea #UmarKamani amefunga ndoa na mwanamitindo kutoka nchini Uingereza #NadaAdelle wikendi hii.

Tovuti ya Daily Mail imeeleza kuwa wawili hao walifunga ndoa na kufanya sherehe iliyo gharimu Pauni 20 milioni na kufanya maonesho ya burudani ya muziki ndani ya siku nne kutoka kwa wanamuziki Mariah Carey na Andrea Bocelli nchini Ufaransa katika hoteli ya Grand Allee.

Kufuatia sherehe hiyo iliyoanza siku ya Ijumaa, Umar na Nada waliwakaribisha marafiki zao mashuhuri, wanamitindo akiwemo Naomi Campbell, mwigizaji Tessa Thompson, mcheshi Russell Peters, mwanamuziki Christina Milian, mhariri mkuu wa Arabia Manuel Arnaut, na Mkurugenzi Mtendaji wa Red Sea Film Festival Foundation Mohammed Al Turki.

Umar mwenye umri wa miaka 36 na Nada mwenye umri wa miaka 31 walikutana mwaka 2020 ambapo waliweza kuchumbiana mwaka 2021 na kuyaweka mahusiano yao hadharani.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags