Mwanamitindo Iris afariki dunia

Mwanamitindo Iris afariki dunia

Mfanyabiashara na mwanamitindo kutoka nchini Marekani Iris Apfel, ambaye anajulikana zaidi kupitia ubunifu wake wa mavazi afariki dunia akiwa na umri wa miaka 102.

Taarifa ya kifo chake ilitolewa na familia yake ambapo walieleza kuwa mwnaamitindo huyo alifariki siku ya jana Ijumaa nyumbani kwake Palm Beach huku sababu ya kifo chake bado haijajulikana, lakini wengi wanasema huenda amefariki kutokana na uzee.

Iris Apfel, aliwahi kuwa balozi wa chapa mbalimbali, mbunifu wa mavazi, pia aliwahi kufanya kazi Ikulu ya White House nchini Marekani akiwa kama mbunifu wa decoration za nyumba ‘Interior designer and fashion’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags