Mwanafa: Watanzania chezeni gofu

Mwanafa: Watanzania chezeni gofu

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwanafa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itahakikisha kuwa inapaza sauti kuhusu mchezo wa gofu ili umma upate uelewa kuhusu umuhimu wa mchezo huo Kitaifa na Kimataifa.

Kauli hiyo ameitoa Jijini Dar es Salaam alipokuwa akihutubia katika hafla ya ufungaji wa shindano la gofu la NBC Lugalo Open 2023 ambapo alialikwa kama Mgeni rasmi.

Aidha ameipongeza Klabu ya gofu ya Lugalo kwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wananchi wote kutumia klabu hiyo kucheza gofu, na kwa kuchukua hatua chanya za kuibua vipaji vya mchezo huo kwa watoto. Pia akaahidi kuiunga mkono klabu hiyo kwa kuipa misaada muhimu inayohitajika.

Chanzo Ayo tv






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags