Udugu ulitolewa valentine au nikuache kidogo sio shida zako, hahahha! Maana wanachuo ndo mambo yenu haya, lakini mwaka huu mmetuangusha sana hampendwi nini (jokes).
Sasa bwana kama tunavyojua wanachuo wengi wako katika mitihani na wengine ndo wanamalizia malizia, najua kutakuwa na kalikizo karefu kidogo kama mwezi mmoja, basi bwana usikubali kukaa tuu nyumbani kizembe zembe, nimekusogezea baadhi ya mawazo ya biashara ambalo utaliona linakufaa basi malizana nalo.
Kama mwanafunzi, unaweza kuwa na muda mwingi wa kujihusisha na shughuli za ujasiliamali. Kuna fursa mbalimbali za kibiashara ambazo wanafunzi wa vyuoni wanaweza kuanzisha bila gharama kubwa ya mwanzoni au kuhitaji kutenga muda mwingi sana.
Maelfu ya wanafunzi wanajichumia mapato kupitia biashara ndogo zenye faida kubwa. Haya hapa ni baadhi ya mawazo ya biashara nzuri kwa wanafunzi
- Kufungua mgahawa( cyber cafe)
Hili ni wazo la biashara la kwanza kabisa ambalo litakusaidia kupata kipato ukiwa chuoni hata ukiwa likizo, ili biashara yako ikuwe Zaidi basi tafuta eneo ambalo liko karibu na chuoni kwenu ili uweze kujua biashara yako inavyotoka.
Kuna baadhi ya wanafunzi wakishafika chuon wanajiita slay queen wanaogopa kufanya biashara kisa watu watamuonaje, hayo ni maisha yako ndugu yangu usiogope wala kuangalia nani kasema nini fanya mambo yako na watu hawajui tuu biashara hii ina faida sana pale tu ukiwa serious
nayo.
- Kufungua duka la kuuza mavazi
Wanafunzi wa vyuoni wanapenda kuvalia nadhifu kwa mtindo wa kisasa, Biashara hii itakuwa na soko kubwa wakati wowote kwasababu wanafunzi wakishaingia chuo hupendelea Zaidi kila siku kuonekana akiwa tofauti mbele ya macho ya watu.
unahitaji tu kufanya utafiti wa mavazi yanayovuma kimtindo na upo tayari kwa biashara hii siku zote wanasema biashara ni moyo, Unahitaji kuwa na duka lililopo katika eneo la karibu na kupata fedha za kutosha ili uweze kuwa na aina tofauti ya nguo na bidhaa za mitindo kutoka kwa wanamitindo mbalimbali.
Iwapo duka halipatikani, unaweza kuuza vitu yako katika eneo wazi, hasa nyakati za jioni. Kwa kufanya hivi utajihakikishia mtiririko wa mapato.
Siku hizi sio lazim uwe na duka, duka unatembea nalo kwenye kwenye simu, hii sio yakusema sijui ufungue duka hapana na sio lazima ukiwa chuo hata ukiwa likizo itakusaidia usiwe dada wa nyumbani.
- Biashara ya ususi
Biashara zinazowalenga wanawake hustawi vizuri, Duka la ususi ni biashara ya faida kubwa sana ambayo mwanafunzi wa kike anaweza kuanzisha. Ni biashara inayohitaji muda mwingi, na inakuhitaji kusawazisha kati ya masomo na biashara. Ili kuwa na wateja wengi, unahitaji kujua mitindo ya nywele inayotrend.
Cha kufanya tuu ni kutafta msichana mmoja wa kazi ambae utasaidizane nae pindi wewe utakapokuwa darasani unaendelea na masomo, jambo la msingi kabisa ni kuwashawishi wanafunzi wenzako wawe wanasuka katika saloon yako.
Tena wakati wa likizo utakuwa free sana na kujua changamoto wanazopata wateja wako kwasababu unakuwa uko nao muda wote katika saloon yako.
- Kufungua duka la wakala
Biashara ya wakala ni yenye ushindani sana Kama chuo unaposomea kuna idadi kubwa ya wanafunzi, kutakuwa na soko kubwa na biashara yako ina uwezo wa kustawi vizuri. Unaweza hata kuchukua fursa hiyo ya kibiashara kwa kuuza vocha, Hebu fikiria kupokea mapato ya kila mwezi kutoka kwa mojawapo ya kampuni husika hii biashara ni yenye faida sana.
Uzuri wa biashara hii si lazima ufungue kibanda bali unaweza kutuma na kutoa pesa ukiwa hata uko class kwasababu vifaa vyako utakuwa unatembea navyo kila sehemu, hii itakusaidia mwenyew kujua leo umeingiza kiasi gani na umetoa kiasi gani.
- Kupiga picha
Kama unapenda kupiga picha, hii ni nafasi yako ya kupata pesa kutokana na shughuli hii. Unahitaji tu kamera, mwanga, vifaa vya kudhibiti mwanga na ujuzi wa kupiga picha. Unaweza kutumia wikendi kwa kupiga picha katika harusi, mikutano, na sherehe mbalimbali.
Unaweza pia kutoa huduma ya kupiga picha na kuziuza kwa familia na watu binafsi. Unaweza pia kuuza picha zako kwenye soko la mtandao kama vile AfricanStockPhoto. Pia unaweza kupata pesa kupiutia wanafunzi wenzio kwa kuwapiga picha.
Hapa sasa ndo utakuwa free kuedit pic za watu kwa Amani na kwa uharaka Zaidi bila yakusumbuana na wateja wako kwa kuzima simu ili tu usome ndo umalize kuwafanyia kazi yao. Na utakuwa unapata watu wengi kwasababu ya kupatikana muda wote.
Aloooooh! I hope tumeelewana fika katika hili mnapo kwenda makwenu hata kama ni vijijini lazima kuna biashara moja itakuwa inakupatia faida kwa kuangalia mazingira. Na nyie mnao amua kubaki hostel kwakua likizo sio ndefu hii itawafaa Zaidi kwasababu mko katika jiji ambalo lina fursa nyingi sana.
Leave a Reply