Mwana Fa: Hakuna Mtawala Kwenye Sekta Ya Uchekeshaji

Mwana Fa: Hakuna Mtawala Kwenye Sekta Ya Uchekeshaji

Kuelekea siku ya ugawaji wa tuzo za Tanzania Comedy Award Tarehe 22 Februari 2025, Naibu waziri wa Habari tamaduni sanaa na michezo Hamis Mwinjuma, Mwana FA amesema tukio hilo nila kihistoria kutokea kwenye tasnia ya uchekeshaji nchini.

Mwana FA ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Februari 17,2025 alipokuwa Mlimani City wakati wa Tamasha la All Stars Comedy Festival.

"Siku ya leo ni siku nzuri kwenye historia kwa sababu ndio mara ya kwanza tunapiga hatua ya kwanza kuelekea usiku wa kuwatunza na kuwaheshimisha wachekeshaji wetu lakini jambo zuri ni kwamba hatuwaheshimishi wachekeshaji wasasa pekee na hata wale wa zamani tunawapa heshima yao na tunawaambia kwamba kazi walio ifanya hatuichukulii poa.

Tunajua wanatuongezea siku za kuishi tunafahamu wanatupunguzia strees zetu yaani kikubwa uwe na bando tu na kweli wanaifanya kazi hiyo vizuri na sisi kutoka serikalini tunawaonesha tunathamini kazi ambayo wanaifanya" Amesema Hamis Mwinjuma.

Mwana FA ameongezea kuwa kama Wizara yao hawahusiki na kuchagua mchekeshaji gani ashinde na nani asishinde lakini pia hilo ni tukio la mwisho kabisa litakalo zingatiwa kuelekea usiku wa ugawaji wa tuzo hizo.

"Nafikiri hilo ni jambo la mwisho kabisa na litakuja wakati tunaenda siku usika wa ugawaji wa tuzo hizo lakini mpambano ni mkali kwa sababu wachekeshaji wengi wamekuwa wakifanya vizuri na hakuna mtawala kwenye sekta hiyo kwamba utaweza kutabiri" amesema Mwana FA.

Hata hivyo, Naibu Waziri huyo amepongeza waanzilishi wa Tanzania Comedy Award chini ya msanii Ommy Dimpoz kwa hatua hiyo ya kuanzisha tuzo kubwa za wachekeshaji Afrika mashariki ambazo hazijawahi kutokea hapo awali.

"Kwanza siamini kwenye nchi za Afrika mashariki na kati kama kuna tuzo za namna hii sisi ni wa kwanza kwaiyo sisi ni mfano wa mambo mengi kwenye muziki tunajua kabisa sisi tunaongoza hali ni hiyo hiyo kwenye komedi na hatuta acha kuwa viongozi, amemalizia Mwana FA






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags