Mwamuzi awaomba radhi Bayern

Mwamuzi awaomba radhi Bayern

Beki wa klabu ya #BayernMunich, #MathiasDeLigt amedai kuwa mwamuzi wa pembeni katika ‘mechi’ iliyochezwa jana Jumatano dhidi ya #RealMadrid amemfuata na kumuomba radhi kwa kukataa goli lao.

Imeripotiwa kuwa baada ya mchezo huo ‘kocha' wa kikosi hicho Thomas Tuchel alitoa lawama kwa mwamuzi huyo kwa kudhulumiwa 'goli' hilo, hali ambayo ilimfanya mwamuzi huyo wa pembeni kumfuta De Ligt kuomba msamaha ambapo amedai kuwa yalikuwa makosa ya kutafsiri vibaya maamuzi.

Bayern walifunga ‘goli’ hilo lililokataliwa na mwamuzi huyo wa pembeni akasema halikuwa goli bali wachezaji wa kikosi hicho walikuwa wameotea.

Mchezo huo uliamuliwa kwa ‘klabu’ ya Real Madridi kuibuka na ushindi wa bao 4-3 huku Baryen wakishindwa kuchukua kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu kumaliza msimu wa pili Bundesliga, ligi ya mabingwa na DFB Pokal.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post