Mwamnyeto: Tutalipa kisasi katika kombe la ASFC

Mwamnyeto: Tutalipa kisasi katika kombe la ASFC

Aloooooooh! Baada ya kulala hoi weekend hii kwa kichapo cha bao mbili mtungi, wananchi wameibuka tena na kusema kuwa wanaamini watalipiza kisasi katika kombe la Azam sport federation cup.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Mwamnyeto campain wa klabu ya yanga amefunguka na kueleza kuwa “ Poleni wananchi kama mnavyojua muda wote tupo uwanjani kuipigania nembo ya wananchi kwa machozi, jasho na damu. Tumeumizwa na matokeo kama ambavyo mashabiki wetu mmeumizwa” ameandika Captain Mwamnyeto

Aidha aliendelea kwa kueleza kuwa “ Ila nawasihi tugange yajayo tuna mechi muhimu ya kuandika historia dhidi ya Rivers United wote akili na dua zetu tuelekeze uko, kisasi ni haki naamini tutakutana na watani wetu kwenye kombe la Azam Sports Federation Cup” ameandika Bakari Mwamnyeto






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags