Mwamnyeto awakosa Al Merreikh

Mwamnyeto awakosa Al Merreikh

‘Klabu’ ya #Yanga kupitia mitandao yao ya kijamii imethibitisha kuwa itamkosa ‘beki’ na nahodha, Bakari Nondo Mwamnyeto wa kikosi hicho ambacho kinatarajia kuondoka nchini leo September 14 na kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ‘mechi’ ya kimataifa ya ligi ya mabingwa dhidi ya Al Merreikh.

Aidha ‘beki’ huyo ataukosa mchezo wa kwanza wa kutafuta mshindi wa kufuzu hatua ya makundi ya Champions League (CAF) dhidi ya Merrikh kutokana matatizo ya kifamilia.

Hata hivyo ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo Miguel Gamondi amempa ruhusa ya kwenda kushugulikia matatizo ya kifamilia hivyo Mwamnyeto ataungana ana ‘timu’ baada ya ‘mechi’ hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags