Mwalimu wa darasa la tatu akamatwa amelewa darasani

Mwalimu wa darasa la tatu akamatwa amelewa darasani

Mwalimu wa darasa la tatu ayefahamika kwa jina la Kimberly Coates, amekamatwa akiwa amelewa darasani katika eneo lake la kazi kwenye shule ya msingi Perkins-Tyron iliyopo Oklahoma.

Mwalimu huyo ambaye ilikuwa siku ya kwanza kuripoti kazini hapo aligundulika kuwa ametumia kilevi, baada ya kuulizwa na afisa wa polisi  alidai kuwa alikuwa ametumia usiku wa kuamkia siku hiyo ili apate usingizi kwani alikuwa na wasiwasi siku hiyo.

Baada ya polisi kumfanyia vipimo aligundulika kuwa ametumia kiwango kikubwa cha pombe na kukiri kuwa alitumia kilevi wakati akiwa njiani anaelekea shuleni hapo, jambo lililopelekea kushikiliwa na polisi kwa kosa la kuingia darasani akiwa amelewa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags