Mwakinyo: Tafuteni walimu wazuri wa ngumi achaneni na waganga

Mwakinyo: Tafuteni walimu wazuri wa ngumi achaneni na waganga

Bondia maarufu nchini Hassan Mwakinyo ametoa ushauri kwa mabondia wengine kwa kuwaambia watafute walimu wazuri wa ngumi.

Mwakinyo amedai kuwa ngumi ni pesa na maisha na sio usela tena hivyo basi ni vizuri kutafuta walimu wazuri wa ngumi na sio kutafuta waganga.

Ushauri huo Mwakinyo ameutoa kupitia ukurasa wake wa #Instagram ameandika,

“Jana nilipokea simu ya shabiki mmoja mwenye hekma sana na mahaba juu ya mchezo wa ngumi akanieleza yakua boxing's is dangerous sport in the world!! you have to be verry carefull serekali kwa maana ya Wizara na Vyombo vya Habari vya Tanzania na baadhi ya na kampuni na watu binafsi wana jitahidi sana kuonyesha ku-support mchezo wetu.

Alhamdulilah na mimi nasema kua Ngumi ni pesa ngumi ni maisha na sio usela tena kama ilivyo zoeleka hii ni fursa tafuteni walimu wa ngumi wazuri wenye weledi wa kweli achaneni na waganga kua mganga mzuri sio kua mwalimu mzuri wa boxing elimu ya boxing sio ya uganga na ramli #ColoradoKingsBigmotion’s bendera puto mlingoti sindanosukudu”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags