Mwakinyo amkingia kifua Dulla Mbabe

Mwakinyo amkingia kifua Dulla Mbabe

Bondia Hassan Mwakinyo ameonesha hisia zake za kutopendezwa na kejeli na maneno ya kashfa yanayoendelea kwa baadhi ya watanzaniaa kwa bondia mwenzake Abdallah Pazi maarufu kama Dulla Mbabe baada ya kupoteza pambano usiku wa kuamkia jana.

Dulla Mbabe alichezea kipigo katika pambano la uzito wa  kati lililopewa jina la ‘Kiboko ya Wageni’ dhidi ya bondia Tshimanga Katompa kutoka Congo.

Pambano hilo la raundi 10 lilifanyika katika ukumbi wa TPA sabasaba jijini Dar es salaam na kushuhudia Dulla Mbabe akipigwa kwa pointi katika pambano hilo.

Akizungumza baada ya pambano hilo, Mwakinyo alisema kupoteza pambano haimaanishi kwamba sio bingwa wala hajui, bali amefanya vizuri kwa kadri ya uwezo wake hivyo anamsapoti na yuko pamoja naye.

“ Umeshinda Ulaya hakuna mtu aliyekuposti wala kukusapoti leo umepoteza kila mmoja nakusema vibaya nikwambie tu mimi niko pamoja na wewe na nitaendelea kukusapoti”alisema

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags