Mwakinyo akana kufungiwa

Mwakinyo akana kufungiwa

Alooooh! Baada ya lile sakata la kusambaa kwa taarifa kuwa bondia maarufu nchini Tanzania Hassan Mwakinyo kufungiwa kupigana nje mwenyewe amefunguka na kusema kuwa hajafungiwa.

Mwakinyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka ujumbe mrefu akieleza kuwa, “Guys naomba niweke sawa kuhusiana na huo uvumi. Mimi sijafungiwa kama wanahabari wanavyo eneza ila “British boxing borde control” ni moja ya sheria yake hairuhusu mchezaji yoyote aliepoteza kwa tko au k o kurudi ulingoni kwa muda wa siku 45 zipite mpaka siku 60, lakini hio haimaanishi mtu huyo kuvunja sheria au kufanya kosa lolote lile ambalo litagharimu yeye kutocheza pale tena,” ameandika Mwakinyo.

Aidha bondia huyo aliendelea kufunguka kwa kuwaeleza Watanzania wenzake kuwa, “nimeweka picha mbili hapo ukiswipe utanielewa na muwe makini na habari hizo mnazo eneza ukiwa mwanahabari wa michezo lazima ujifunze kujua sheria kabla kuongelea jambo Asalaaam alaykum,” ameandika Hassan Mwakinyo.

Duuuuuh! Dondosha komenti yako hapo chini una yapi ya kumwambia bondia huyu na je kwa wale wataaramu wangumi hii ilo sahihi au laaaah!.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post