Mwakinyo ajutia usingizi wake

Mwakinyo ajutia usingizi wake

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Hassan Mwakinyo ameeleza kuwa anajutia usingizi wake huku akidai hakuna ushindi wa namna ile, hii ni baada ya kushuhudia pambano la Twaha Kiduku lililofanyika usiku wa kuamkia leo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram #Mwakinyo ameshusha ujumbe ulioeleza kuwa…

“Najutia usingizi wangu, yani leo umeonesha kuwa wewe hauna sifa wala vigezo vya kuwa pro nimekua kwenye boxing kwa takribani miaka 17 sasa, hakuna ushindi wa namna ile Kibenju nertwork ya Mlundwa imekubeba sana kutafuta bondia wa kuja kuachia na hii ndiyo salama yako kama sio ofa na jamaa angeamua kukaza angekuvua nguo tena.

Kiwango chako ni kibovu sana siku hadi siku haukui ki mchezo Simba na Yanga zinafuzu kila siku na zinabadilisha walimu wewe unapigwa kila siku lakini ni kama umefunga nae ndoa listen ukitaka kujilinganisha sawa na mtu kwa ubora make sure baadhi ya vitu mnafanana au unakuwa zaidi yake. Asalaam Alaykum”

Ikumbukwe kuwa usiku wa kuamkia leo mkoani #Morogoro katika ukumbi wa Tanzanite kulikuwa na pambano kati ya Twaha Kiduku na Harpreet Singh kutoka India, ambapo kufuatia na pambano hilo Kiduku aliibuka mshindi kwa kumchapa Singh kwa #TKO raundi ya tano.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags