Muundo wa kituo cha treni wazua gumzo

Muundo wa kituo cha treni wazua gumzo

Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini China wamestaajabishwa na muundo wa kituo kipya cha treni, kituo hicho kufananishwa na taulo za kike (pedi).

Muundo huo uliyopendekezwa na kituo cha Nanjing Kaskazini ulitolewa wiki chache zilizopita ambapo uliripotiwa kugharimu dola 2.7 bilioni sawa na Sh 7 trilioni.

Aidha wabunifu hao waliweka wazi kuwa wazo la kubuni muundo huo lilikuja kutokana na maua yaitwayo ‘Plum’ ambayo ni maarufu sana katika jiji hilo la Nanjing.

Hali ilikuwa tofauti kwa wananchi ambapo walienda mitandaoni na kufananisha muundo wa kituo hicho kama taulo za kike.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags