Muonekano wa Jackie Chan , wagusa hisia za mashabiki

Muonekano wa Jackie Chan , wagusa hisia za mashabiki

Picha za mwigizaji Jackie Chan zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, zimezua gumzo baada ya nyota huyo kuonekana akiwa ameota mvi kichwani na kwenye ndevu.

Picha hizo alizopiga akiwa Sichuan, china zinaonekana kuzua hisia kutoka kwa watumiaji wa mitandao huku wengi wakishangaa muonekano wa uzee wa mkali huyo.

Kwa sasa Jackie Chan ana umri wa miaka 69, alizaliwa mwaka 1954 Victoria Peak, Hong Kong. Alianza kucheza katika filamu maarufu ya Bruce Lee Enter the Dragon na baadaye akawa msanii mkubwa. Aliwahi kutunukiwa tuzo ya heshima ya Oscar mnamo 2016.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post