Mummy Huki na Biashara ya Urembo

Mummy Huki na Biashara ya Urembo

Na Aisha Lungato

Katika maisha kuna kile kitu ambacho binadamu hukipendelea zaidi. Wadada wengi kama ilivyo ada hupendelea zaidi urembo, nikizungumzia urembo na maanisha kuwa na muonekano mzuri kuanzia juu mpaka chini.

Kwa miaka ya hivi karibuni wakina dada wengi huonekana kuvutiwa zaidi na maswala ya kujipodoa yaani kupaka make-up na kuwa “Make Up Artists.”

Licha ya kuwa na make-up artists wengi miaka ya hivi karibuni, bado imeonekana kuwa mabinti wengi na wadada wengi huendelea kuvutiwa na urembo huo hadi kuchukua jukumu la kwenda kujifunza kuwa make-up artists.

Imezoeleka kuwa binti au kijana akiwa katika masomo hatakiwi kujihusisha na mambo mengine bali kuzingatia masomo tu, lakini kwa karne hii wanafunzi wengi wameonekana kujishughulisha zaidi kwa kufanya biashara angali wakiwa bado wanasoma, ili waweze kujikimu katika maisha yao na kuacha kutegemea wazazi wao na kufanya maendeleo.

Vivyo hivyo kwa binti ambaye ana muonekanano mdogo sana, Mummy Huki ambae ni mwanafunzi wa chuo cha The Institute Finance of Management (IFM), mwaka wa tatu, akisomea kozi ya Bachelor of Science in Economic and Finance.

 

Licha ya kuwa mwanafunzi, Mummy aliamua kuwa mfanya biashara ya urembo, yani kuwa “Make-up Artist,” pia anajihusisha na ujasiriamali wa kuuza vitu mbalimbali vinavyotumiwa zaidi na kina dada kama vile hereni, cheni, na nguo.

Hivi karibuni Mummy amefungua salon mbili ambazo amezipa jina la “Mummy Beauty Parlour,” salon ambazo zote zinafanya kazi ya kutoa huduma za urembo kama vile kupaka make-up, kusuka na kusafisha kucha, pia amefanikiwa kuwaajiri vijana wenzake ambao wanachangamoto za ajira, ili waweze kusaidiana katika biashara hiyo kipindi ambacho anachokuwa katika masomo yake. Vijana hao ndio husimamia salon zote na kazi za ofisi hiyo anapokuwa darasani.

KWANINI ULIAMUA KUFANYA BIASHARA YA MAKE-UP NA SIO BIASHARA NYINGINE?

Binti huyo alifunguka kwa kusema kuwa aliamua kufanya biashara hiyo kwa sababu ni kitu ambacho alikuwa akikipenda sana toka alivyo kuwa mdogo.

Aliendelea kwa kueleza kuwa kipindi yuko mdogo alipendelea sana kuwa model na kudizaini nguo lakini alivyoendelea kukua zaidi alijikuta akipenda zaidi kupamba watu.

Hata hivyo ameeleza kuwa haikumuwia vigumu kufanya biashara hiyo kwakua alikuwa akiipenda toka akiwa mdogo, hata hivyo hakuwahi kusomea wala kujifunza sehemu yoyote ile.

Ameeleza kuwa ni kipaji tuu alichojaaliwa na Mungu, na kadri alivyoendelea kupaka watu make-up, aliendelea kuwa bora zaidi mpaka kufikia kupamba maharusi.

Hata hivyo, Mummy amefunguka kuwa biashara hiyo inamsaidia zaidi katika kujikimu katika maisha yake kwani kipato kidogo anachokipata, husaidia familia yake na kufanyia maendeleo yake kwa ujumla. Faida nyingine anayoipata kupitia biashara hiyo ni kukutana na wafanyabiashara wakubwa na kushauriana mambo makubwa zaidi ya kibiashara.

“Kwa sasa mimi sio tegemezi kwa wazazi wangu, najilipia mwenyewe kodi ya pango, najinunulia mwenyewe chakula na kufanya kila ninacho kitaka, nataka kuwaeleza tu vijana wenzangu kwamba pesa ya kutafuta mwenyewe ni tamu sana, yaani pesa ya jasho lako ni tamu, so epuka pesa ya masimango.”

Mummy anawashauri vijana kuacha kubweteka na kutegemea wazazi au kutegemea ujuzi wanaosomea na kuamka kufanya kazi na biashara kwa ujumla anaamini kila binadamu ana kipaji na anawashauri vijana watumie vipaji vyao na wavifanyie kazi ili waweze kutimiza mahitaji yao mbalimbali.

Pia ameongezea kwa kusema kuwa vijana waweze kuchanganyika na watu mbalimbali ili waweze kupata mawazo mbalimbali ya kimaendeleo.

 “Vijana wengi wa siku hizi wanapenda sana photoshoot na kuchat, hivyo vitu vipo cha kuwaambia tuu ni tufanye kazi, tuwataftie watoto wetu waje kuishi maisha mazuri ambayo sisi hatujabahatika kuyaishi, tuwatengenezee misingi bora,” alisema.

Binti huyo amefunguka zaidi kwa kusema kuwa kitu ambacho anakipenda zaidi ni kufungua kampuni kubwa ambayo itajulikana msanii na nje ya Tanzania itakayo husishwa maswala mazima ya urembo kama vile modelling, designing na uuzaji wa vipodozi  na kuzalisha vipodozi vyake mwenyewe na kuwa na brand yake mwenyewe

Mummy pia anatamani kuwa kama Dc wa Temeke, Mheshimiwa Jokate Mwegelo, kwasababu anamuinspire sana kwa kazi anazozifanya katika nchi yetu na taifa letu kwa ujumla.

Pia anatamani sana kuwa mfanyabiashara na afisa mkubwa sana ndani na nje ya Tanzania, huku akieleza kuwa akimaliza Degree yake ya Economics and Finance, ataunganisha Masters ya Economics and Finance.

“Kama unahitaji kufanikiwa na kufika mbali inabidi uache kusikiliza watu wanasema nini na ufocus katika jambo lako, pia usikubali mtu yeyote akukatishe tamaa, simama pambana. Sisi vijana ndio taifa na maendeleo ya baadae, tufanye kazi tufanye biashara ili tuifike mbali kimaendeleo na pia jitahidi kutafuta marafiki wenye mawazo chanya sio marafiki kila siku wanawaza mtaendea kula bata wapi, tafuta marafiki wenye kupenda maendeleo,” aliongeza.

Nje ya kusoma na kujishughulisha na biashara ya make-up, Mummy ni mtangazaji wa radio ya Magic Fm, katika kipindi cha DalaDala Beat, kwenye segment ya University corner, kipindi ambacho hutoa burudani na elimu kuhusu mambo mbalimbali kama vile biashara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags