Mume wa Cassie atoa ya moyoni

Mume wa Cassie atoa ya moyoni

Baada ya video ya Diddy ikimuonesha akimpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie kuvuja na kusambaa katika mitandao ya kijamii, na sasa mume wa Cassie, Alex Fine ameyatoa ya moyoni huku akiweka wazi kuwa kuanzaia sasa atawaunga mkono wanawake wote waliyokutana na mateso ya Diddy.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Fine ame-share video hiyo inayoendelea kusambaa kupitia mitandao ya kijamii ikiambatana na ujumbe uliyokuwa ukieleza kuwa Wanaume wanaopiga wanawake si wanaume huku akiamini kuwa wote waliyomfungulia kesi Diddy kuwa kesi hizo ni za kweli.

Hata hivyo Fine alimalizia kwa kueleza kuwa kwa sasa Diddy hayupo salama tena kwani wale watu wake wote wa karibu aliyokuwa akiwategemea tayari wamemtenga.

Cassie na Fine walidaiwa kuwa wapenzi Desemba 2018, miezi miwili baada ya Cassie kuthibitisha kuachana na Diddy ambapo wawili hao walifunga ndoa Agosti 2019 na kubahatika kupata watoto wawili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags